Alhamisi, 22 Machi 2018

Madiwani wa halmashauri ya jiji la dar wahoji mapato ya soko la kariakoo

Madiwani halmashauri ya jiji Dar wahoji fedha zitolewazo na soko la Kariakoo
Uhakika daily · 
BARAZA la Madiwani wa Jiji la  Dar es Salaam limeomba kufahamu kiasi cha fedha kinachopatikana katika Soko la Kariakoo maana wamechoshwa na kauli ya kwamba soko hilo linaendeshwa kwa hasara.

Baadhi ya madiwani hao wamekiambia kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji hilo leo jijini Dar es Salaam wamesema Jiji linamiliki soko kwa asilimia 51.Diwani wa Kata ya Mbezi Humphrey Sambo amekiomba kikao hicho kupata taarifa za mapato ya soko hilo kwani kwa mtazamo wa kawaida wamedai fedha inayopatikana ni nyingi lakini wao wanaambiwa linaendeshwa kwa hasara.

"Tufuatilie ili kujua nini ambacho kinaendelea katika Soko la Kariakoo kwani nimechoka kusikia kila siku wanapata hasara lakini watu wanakwenda kazini," amesema.Amefafanua kwa kuwa Jiji linahisa ya asilimia 51 ni vema ikajulikana kinachopatikana na mgao wa Jiji ni kiasi gani.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Tabata Patrick Asenga amesema soko la Kariakoo si kweli linapata hasara kwani hata vizimba vya biashara vilivyopo kodi yake ni Sh.300,000 hadi Sh.400,000.Amesema ni vema Jiji likatoa kauli ya kuwaita wanaosimamia soko hilo ili waeleze kuhusu soko hilo na kwamba hakubaliani na kauli ya soko kuendeshwa kwa hasara.

Kutokana na maelezo hayo ya madiwani,Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amemuomba Mkurugenzi wa Jiji hilo kuyafanyia kazi na kwenye kikao kijacho majibu yatolewe."Mkurugenzi wa Jiji naomba ukae na menejimenti yao  kushughulikia suala hili kwanza na  na menejimenti yake na baada ya hapo taarifa itolewe," amesema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

West Africa

West Africa In the western Sahel the rise of settled communities occurred largely as a result of the domestication of millet and of ...